MKUTANO WA INJILI 2025
LAMADI – SIMIYU
LAMADI
SIMIYU
JUNE 18-22, 2025
LENGO
Kwa neema ya Mungu lengo letu ni kufikia angalau 10% ya wakazi wote wa Lamadi yaani watu 5,000 Kupitia shughuli mbalimbali za Unjilisti, umisheni, huduma za kijamii, misaada ya kibinadamu n.k.
Kati yao angalau watu 500, wafunguliwe na waokoke (wamkiri na kumpokea YESU KRISTO kuwa BWANA na MWOKOZI wa maisha yao).
#LAMADI INAFIKIKA
#LAMADI IMEFIKIWA
FAMILY GOSPEL OUTREACH MISSION 2025
Kuhusu Lamadi
JE WAJUA?
Lamadi ni mji Mdogo na Kata katika Wilaya ya Busega, Mkoa wa Simiyu, Tanzania
- Iko kando ya Ziwa Victoria (Magharibi), na unapakana na Wilaya ya Bunda (Kaskazini) na Pori la akiba Kijereshi (Masharki)
- Km 130 kutoka jijini Mwanza (masaa 2 kwa gari)
- Inafikika kwa barabara ya lami ya Mwanza- Musoma, Shinyanga-Bariadi- Lamadi.
- Mabasi yote ya Kutoka Dar, Dodoma kwenda Musoma yanapita Lamadi.
- Kutokea Arusha/Moshi unaweza kufika Lamadi kupitia Musoma au Mwanza.

Mitaa ya Lamadi
Mitaa yake ni Itongo, Makanisani, Majengo, Msekula Road, Mwalukonge, Kisesa na vijiji vitatu ambavyo ni Lukungu, Mwabayanda na Kalago (Mwabulugu Lakeshore).
Idadi ya Watu
Jumla: 44,146
Wnaume: 20,470 (46%)
Wanawake: 23,676 (54%)
Idadi ya Kaya : 9,553
Wastani wa watu katika Kaya: 4.6
Chanzo: Sensa ya watu na Makazi (2022)
Idadi ya Makanisa
Kipentekoste (CPCT): 17
Mitume & Manabii: 10
Protestanti: 6
Roman Katoliki: 2
Adventista wasabato (SDA): 5

Upagani + Ushirikina
Kwa wastani, Lamadi inakadiriwa kuwa na waganga wa jadi wengi (200) kuliko Wachungaji (makanisa yote 40).
Hii inaonesha ni eneo lenye uhitaji mkubwa wa INJILI. Kuvunja nguvu na madhabahu za ushirikina na upagani.
Hitaji la Injili
Wakristo waliokoka wanakadiriwa kuwa 3,500 sawa na 8% ya wakazi wote (44,146).
Wakazi wote ambao angalau wanahudhuria ibada makanisani (makanisa yote) wanakadiriwa kuwa elfu 10 (22.4%).
Inakadiriwa kuwa zaidi ya wakazi elf 34 (sawa na 77.5% ya wakazi wote) ni WAPAGANI- Hawajampokea YESU na wala hawashiriki Ibada makanisani.
Hii inaonesha Ni eneo ambalo halijafikiwa kwa kiwango cha kutosha na lina uhitaji wa INJILI kwa kiasi kikubwa.
Changamoto za Lamadi
KIJAMII
Mji wa Lamadi umetawaliwa na roho ya uasherati, jambo linalosabisha kuvunjika kwa ndoa nyingi, ongezeko la watoto yatima, mauaji ya watu kwa imani za kishirikina, matumizi makubwa ya chuma ulete, Ulevi wa pombe, nk.
KIUCHUMI
Lamadi ni mji wa kibiashara lakini mfumo wa uchumi umetawaliwa na ushirikina wa kiwango cha juu, utoaji kafara, jambo linalosababisha matajiri wanainuka kwa kipindi kifupi halafu wanafilisika.
- Kiwango cha umasikini ni kikubwa; Mkoa wa Simiyu ni miongoni mwa mikoa 5 yenye kiwango kikubwa cha umasikini wa kipato na wa chakula.
- Wastani wa kiwango cha umasikini kwa mkoa wa Simiyu ni 39.2 ambao ni zaidi ya wastani wa kitaifa (26.4) (NBS, 2018)
- Wakazi wengi wanaishi kwa kipato cha chini ya dola moja kwa siku. Wakazi wengi wa Lamadi wamejumuishwa katika Mfuko wa Maendeleo ya Jamii wa kunusuru kaya masikini (TASAF).
KIIMANI/KIROHO
Watu wengi wanapohamia Lamadi hujikuta wamekuwa wapagani; hata kama walikuwa wanashiriki ibada makanisani (maeneo walikotoka). Wakazi wengi walihamia hapa wakiwa hawajawahi kuchanjwa chale kwa mganga, lakini mara tu bada ya kuingia kwenye mji huu wanajikuta wameenda kwa waganga wa jadi, wamechanjwa chale na wamepewa “mafurushi ya mizigo” ambayo hawakuwahi kubeba kabla ya kuhamia Lamadi.!
Takwimu za Uhitaji “Vulnerability” za Mkoa wa Simiyu ambazo zinaweza kutumika kwa Lamadi
-
Kaya zinazoongozwa na wanawake 42.5%
-
Wajane 5%
-
Watoto yatima 10.5% (ya watoto wote chini ya miaka 18)
-
Kiwango cha Ulemavu 9.1% (ya watu wote).
-
9.1% ya kaya zote hazina vyoo
-
Kiwango cha uandikishaji shule za msingi 76%
-
Kaya zinazotumia nishati ya umeme 15.9%
-
Kaya zinazotumia maji ya bomba 34.9%
Chanzo: Sensa ya watu na makazi 2022